Saturday, 2 November 2013

Hii ndo hali halisi kati ya promota na wasanii

     
       Hii ndo hali halisi kati ya promota na wasanii

 Ninaishi kupitia muziki na muziki ndo kazi yangu na ninajituma kweli kweli,juhudi zangu hadi raia wanazijua na ninagharamia biashara yangu kwa fedha muda,mazoezi ubunifu n.k na ninapofuatwa na promota inakuwa hivi!

Promota; sasa sister nina kashoo kangu kamoja ninataka ukaperfom kidogo, dah hivi unajua wewe ni mkali mno na kazi zako zina quality nzuri mno ila usinifanyie bei kubwa sana.

Msanii; okay haina tatizo charity shows ni m1 kama ni local sana hadi laki 8 na show za kawaida dar 1.5 hadi 3 na za nje ya TZ
Promota; eh sister kumbe una price list kabisa dah! lakini kama vipi nisaaidie ndugu yangu hivi unajua watu wanakukubali sana?
Msanii; Mh! hebu niambie wewe unakiasi gani?
Promota; Dah sister nipunguzie basi kidogo ndugu yangu
Msanii; okay nikupunguzie bei ipi ya kwanza ya pili ama ya tatu? 
Promota;Dah sijui nisemeje ila mimi bwana kusema ukweli nina laki tatu ndugu yangu tufanye kama unanisaidia tu nikupe japo nauli tu!
Msanii; je unataka niperfom kwa dakika ngapi/
Promota teh teh teh kama 20,30 hivi aah sistaaa
Msanii; sawa basi utalipa dancers,utagharamia gharama za ukumbi wa kufanyia mazoezi, nauli za dancers maji na msosi, mavazi ya siku ya show na unipatie hiyo nauli unayosema.


Promota; mimi sihitaji kujua hayo mengine hayanihusu wewe unaringa sana,unajiona babkuubwa wakati nilikuwa ninakusaidia tu,kwanza bongo hujulikani huna hata hit song moja.

          Hawa ndo mapromota wetu wengi jinsi walivyo wanasahau kuwa mbali na hayo huwa tunatumia muda mwingi kutunga na kubuni,tunalipia muda wa studio ili tufanye audio kima cha chini 300,000 usafiri,simu,maandalizi labda 150,000 then baada ya hapo kukawa na mtu umemshirikisha gharama nyingine, bado kuna usambazaji wa kazi labda 200,000 kwa ndani na nje ya Tz na video moja kima cha chini 1.5 bado video queen bado hajalipwa location,make up,mavazi,salon tuseme kama milioni 3hvi video ikiisha ufanye usambazaji tena labda 200,000 jamini hii ni haki na halali kweli kwenye kazi za wenzenu? hii mimi huichukulia kama dharau kubwa tena hizo dk 20 hautaimba wimbo mmoja kwenye shoo ya dakika 20 kwa kuwa hata ukimba wimbo mzima ni dk 3 hadi 4 je faida ipo wapi hapa?

Tunafanya biashara hii ili tuweze kujikimu kimaisha tulipe kodi za nyumba,tujenge na mahitaji mengine yote na pia hii ni moja ya sababu wasanii wengi wa bongo huonekana wanatembea tu jukwaani kwa kuwa wanapewa pesa ya kuunga unga na wanafanya show za kunga unga zinazolingana na pesa wanayopewa, ndo maana mashabiki hawaridhiki na show na kuwaona artists si wabunifu na hawajitumi but kiuhalisia ni waandazi wanahusika kwa kuandaa cheap shows kwa kulipa cheap money u get cheap perfomances too, kungekuwa kunampunga wakutosha ninahakika hakungekuwa na msanii yeyote atayezurula jukwaani!   ukitaka show kali 0753320009

2 comments: