Monday, 6 August 2012
Mississippi River
By
Unknown
•
Monday, 6 August 2012
•
0 Comments
Tsup ma pipo hapa nilikuwa New orleans na nyuma yangu ni Mississippi River ambapo tulienda kutupia lunch,wao New Orleans huwa hawatumii mashariki,kusini,magharibi, kaskazini bali huwa wana tumia kusini mwa mto kaskazini mwa ziwa basicly n.k hawa jamaa wamezungukwa na maji na ndo usafiri wao mkubwa kuingiza na kutoa bidhaa nchini interms of bussiness ukifutiwa na train japo ndege zipo pia, Mkazi mmoja aliyekuwa akitutembeza maeneo mbali mbali mjini New Orleans yakiwemo yale yaliyo athirika na catrina alitoa ushuhuda kwamba yeye nyumba yake huwa inakuwa kama inadidimia pindi kina cha maji kikishuka nchini humo na huwa inarudi na kukaa kwenye level sahihi endapo kina cha maji hayo kikitengamaa na kuirudisha ardhi ya nyumba hiyo juu tho kuna wasi wasi ya kwamba endapo maji ya mto huo pamoja na ziwa yakishuka sana kuna uwezekeno maji ya bahari yakaingia kwenye maji hayo ambapo yaweza leta athari kubwa sana nchini humo kwani maji yao yote yaweza kuwa ya chumvi, kwa kuwa pamoja na kutumia mito na mwaziwa hayo kwa kufanyia biashara bali hutumika pia kwa matumizi mengine ya kijamii kama kunywa,kupikia,kufulia N.k
0 comments:
Post a Comment