The Real Ricky ross And Witnesz The Fitnes
Niliye kuwa nae anaitwa freeway Ricky Ross ndo jamaa
aliyemshitaki Rapper Ricky Ross kwa kutumia jina lake,image n.k pamoja na
juhudi zake hizo Freeway Ricky Ross hakuweza kufanikiwa kupata kile anachodai
ni haki yake,kwa kuwa alikutwa na rekodi ya kutumikia kifungo cha maisha jela
kwa kesi ya kutengeneza dola za kimarekani million 600 kama mauzo ya madawa ya
kulevya mnamo mwaka 1980, na kukata rufaa kati kati ya miaka ya tisini ambapo
akapewa kifungo cha miaka 20 badala ya kifungo cha maisha, na hii ni moja ya
sababu kama siyo sababu kuu iliyomkosesha Freeway Ricky Ross haki ya madai ya
kuwa mmiliki halisi wa jina hilo huku mjini Los angeles tukiwa kwenye West
Coast Hip Hop Awards alikuwa akitambulishwa kama The Real Ricky Ross, ambapo
kiuhakika pamoja na hayo jina lake halisi linafahamika kama Ricky Donell Ross
na Rapper Ricky Ross akiitwa William Leonard Roberts II
Pamoja na hayo haikumkatisha tamaa The Real Ricky Ross akaamua
kukata rufaa katika ngazi ya wilaya juu ya maamuzi ya kesi hiyo na kesi bado
ipo mahakamani kwa uchunguzi zaidi, kwa sasa Real Ricky Ross ana miliki Record
Label Iitwayo Freeway Enterprise,Inc na pia anafanya shughuli za kijamii kwa
kupitia mtandao wa internet za kusaidia vijana kwa kuwapa muongozo ya jinsi
gani ya kuishi kiusahihi na kutopoteza muda wao jela na ndiyo maana kwa sasa The
Real Ricky Ross anaandaa movie inayohusu maisha yake kiujumla pamoja na harakati
za kila siku na maisha ya jela baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya so for
now amepata a second chance na hataki kuichezea ambapo alitoka jela September 2009
hadi sasa anawasanii wakali wa kutosha kiasi cha wao kuweza kufanya ziara ya
nchi nzima na ambapo ndo pahala walipokuwa wametoka kabla ya kuja kwenye tuzo
hizo za West Coast Hip Hop awards 2012.
0 comments:
Post a Comment