Fid Q kushoto, Ay kulia akifuatiwa na Witnesz Tz ama the fitnes pamoja na Mwana Falsafa kulia
FID Q AY
WITNESZ MWANA F.A

Ijue sababu ya wasanii wengi wa bongo kulalamika juu ya ,fid Q, Ay, Witnesz, na F.A kupeana madili ya nje ya nchi,
sababu kubwa si kupeana kama wanavyodai raia wengi suala ni kwamba wasanii wengi ni wavivu na si wachangamkia dili na hawako sharp wanajivuta mno,nitakupa mifano miwili;
Mfano A;
Kuna wakati niliwahi kutangaza kwa njia ya redio jamani kama kuna wasanii wowote wale, ambao wangependa kujua ni namna gani anaweza kupeleka video zake chanel o,anaweza nitafuta au anicheki hewani nitamuelekeza, alinicheki msanii mmoja tu jina (kapuni) naye pia baada ya kumuelekeza alitaka nikamchukulie fomu nimpelekee, japo mwingine ambaye alifanikiwa kutuma kwa kupitia ujmbe kama huo ni Black rhino (black chattah) na kufanikiwa kwenda kwenye tuzo za chanel o music video awards'
Ambapo huwa mara nyingi ndo designers wengi huwa wanatambulika kwa faida zao wenyewe kwa kupitia mfumo huu,na niliporudi nika muapproach moja ya wanamitindo wetu nikidhani nitasaidia si kupeperusha tu bendera ya Tanzania kwa kutumia kipaji changu bali hata kuwasilisha sanaa hiyo ya wanamitindo wetu wa bongo,mambo yalienda ndivyo sivyo,kiufupi nilivunjika moyo sana tu baada ya kuambiwa nitoe pesa ya material Dah! nguo nitakazo zitangaza zake,jina nitakalo litangaza lake kwenye red carpet hizo kwa kumnadi na bado anataka nimpatie pesa za material, na endapo wangejua ya kuwa video zetu za muziki ni njia moja wapo kubwa madesigner wengi wanajulikana duniani kupitia mfumo wa kuzidhamini video za muziki na filamu na huwa wanawafuata wenyewe artist wanaodhani watawawezesha na wanaofanya vizuri kama njia moja wapo ya kutangaza na kujiongeza katika biashara yao hiyo ya ubunifu wa mavazi ninaishia hapa kama ni mwanamitindo wa bora elewa na kama bora mwanamitindo ishia hivyo hivyo na kutegea pesa za material!
Mfano;B
Nilikuwa ninaenda tena kwenye tuzo za chanel o mjini afrika kusini kuna jamaa yangu mmoja yeye ni mganda amefungua kituo cha redio kwa njia ya mtandao aitwae kaunda ,aliniomba nimpelekee nyimbo za wabongo amefungua kituo hicho ajiri ya kupiga nyimbo za afrika mashariki zaidi kama kawaida yangu ya kutokata tamaa nikatangaza redioni usiku asubuhi yake tu AY alikuwa ni wa kwanza kuniletea cd yenye audio zake, na wasanii wengine waliahidi kuniletea mpaka nikaondoka,na sikuwaona tena, je tunapendeleana kweli ama tunajua tunachotaka na kuthamini tulicho nachona biashara yetu kiujumla??Hii ni sawa sawa na kuogopa kuingia supermarket wabongo wengi wanatabia hiyo, kwa kuogopa bei kuwa ni kubwa kisa kiyoyozi lakini kiuharisia supermarket ni masoko ambayo yenye usafi wa hali ya juu na yenye bidhaa zilizokaa kwenye mpangilio mzuri na hakuna kupunguziana bei lakini kuna vitu vingine ni bei chini sana na wakati mwingine kila supermarket huwa ina vitu vyake vya bei ghali na ya bei ya chini na kila supermarket ina sifa yake kama sokoni kariakoo,mwananyamala manzese, ilala N.k
Unafanya vyema sana Witness, Lakini naamini unamoyo wa kiujasiliamali
ReplyDeleteSifa mojawapo ya mjasiliamali ni kutokata Tamaa, maanayake ni kwamba nakupa moyo uendelee kuwahimiza kwasababu ili mabadiliko yatokee, anapaswa mmoja amwage damu kwaajiri ya wengi... mimi binafsi naamini wewe utaumia kwaajiri ya wengi na jina lako litakumbukwa
Thanks silvanus I highly apreciate it!
ReplyDeleteGood stuff witness, congrats and keep on keeping on lady!
ReplyDelete